IJUE HOMA YA INI NA NAMNA YA KUJIKINGA

Posted on: July 29th, 2024

Homa kali  ya ini ni nini?

Homa ya Ini ni kuvimba kwa ini. Kitendo cha ini kuvimba ghafla ndio ndio huitwa Homa kali ya Ini. Sababu zinazofahamika zaidi za ini kuvimba ghafla ni maambukizi ya virusi vya homa ya ini aina A na E na ni katika matukio machache sana virusi vya homa ya Ini B na C. Aina fulani za dawa za matibabu ambazo zina sumu zinaweza pia kusababisha homa Kali ya ini. Mara nyingi inaweza kupona bila hata madhara makubwa au kuhitaji matibabu lakini katika matukio machache huweza kusababisha ini kushindwa kufanya kazi na wakati mwingine kifo.

Zipi dalili za homa kali ya ini?

Bila kujali visababishi, dalili za homa kali ya ini ni pamoja na:

-          Kutapika, kuhara au maumivu ya tumbo

-          Rangi ya manjano kwenye macho na ngozi.

-          Choo kilicho na rangi mpauko.

 

Je homa kali ya ini ni tishio kwa maisha?

Kwa kawaida, homa kali ya ini inaweza kupona bila hata madhara ya hapo kwa hapo Katika baadhi ya wagonjwa, maambukizi ya homa kali ya ini aina B au C yanaweza kusababisha maambukizi sugu na kusababisha kovu, ini kushindwa kufanya kazi au hata saratani. Homa kali ya ini inakuwa mbaya zaidi kwa watu wazima kuliko watoto. Watu wazima huonesha zaidi dalili za ugonjwa kuliko watoto na madhara makubwa zaidi ya ugonjwa huo ni kwa watu wenye umri mkubwa.

Idadi kubwa ya watoto huwa hawaoneshi kabisa dalili na ni wachache sana ambao Ngozi na macho hubadilika rangi na kuwa manjano. Inaweza ikaisha haraka bila matibabu au huduma maalum, lakini kuna wakati inaweza kusabaisha ini kushindwa kufanya kazi au kifo. Kunawa mikono kunaweza kuepusha mtoto kuambukizwa homa ya ini aina A na E.

Iwapo una hofu ya kwamba mtoto wako ana dalili za homa kali ya ini, tafadhali onana na daktari ili upate ushauri wa jinsi ya kumpatia mtoto wako huduma anayohitaji.

Je nini kinafahamika hadi sasa kuhusu homa kali ya ini isiyotambulika ambayo imekumba watoto wenye umri wa chini ya  miaka 10 katika nchi kadhaa?

Hadi tarehe 20 mwezi Mei mwaka 2022 kumekuweko na wagonjwa shukiwa wa homa kali y aini 566 na sababu za maambuizi hazijulikani. Na wagonjwa hao wanatoka nchi 33. Nchi mbili zenye wagonjwa wengi ni Uingereza, wagonjwa 197 na Marekani wagonjwa 180. Tunafahamu kuwa ugonjwa huu miongoni mwa watoto unaibua hofu kubwa kwa wazazi na walezi. WHO inachukua suala hili kwa umakini mkubwa na inashirikiana na serikali kubaini chanzo na sababu.

Nini chanzo cha homa kali ya ini miongoni mwa watoto?

Hatufahamu kinachosababisha ugonjwa huu miongoni mwa watoto. Kila mwaka ugonjwa huu hutokea. Kwa sasa bado idadi ya wagonjwa ni ndogo. Wagonjwa wa homa ya ini miongoni mwa watoto hubainika kila mwaka, lakini tunajaribu kubaini iwapo mwaka huu kuna wagonjwa wengi zaidi au la. Baadhi ya nchi zimeripoti idadi ya wagonjwa ni kubwa kuliko ilivyotarajirwa.

Tunachunguza sababu mbalimbali, baadhi kupitia maambukizi au bila maambukizi. Hadi sasa hakuna hata mgonjwa ambaye chanzo ni virusi vya homa ya ini aina ya A, B, C au E. Hakuna pahala mahsusi, chakula, dawa, mnyama, kimelea au virusi ambaye anasema mafua au homa ya dalili viitwavyo adenoviruses. Tunachunguza pia iwapo wagonjwa wa Homa ya Ini wanaweza kuhusiana na ugonjwa wa coronavirus">COVID-19. Bado tunaendelea na utafiti. 

Nini kifanyike kulinda watoto?

Hadi pale tutakapofahamu sababu na chanzo cha ugonjwa huu, ndipo tunaweza kufahamu jinsi ya kujikinga. Njia bora zaidi kwa sasa ni kuchukua hatua rahisi za kulinda watoto dhidi ya magonjwa yanayoambukiza ikiwemo COVID-19:

  • Nawa mikono yako mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji au vitakasa mikono na hakikisha unasimamia watoto nao wafanya hivyo.
  • Epuka maeneo ya msongamano na hakika uko umbali salama kutoka kwa wengine.
  • Hakikisha nyumba ina madirisha ya kupitisha hewa ya kutosha.
  • Vaa barakoa kuziba pua na mdomo.
  • Jikinge pindi unapokohoa au unapopiga chafya.
  • Kunywa maji safi na salama.
  • Iwapo unaugua salia nyumbani na muone daktari    
  •  HII IMETOLEA NA WHO KUPITIA UKURASA WA UN