objective

Matarajio ya hospitali

 1. Kuongeza baadhi ya huduma zitakazokuwa zikitolewa katika hospital yetu ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda hospital kubwa kama Bugando na Muhimbili
 • Huduma za kibingwa za mifupa
 • Huduma za magonjwa ya ngozi
 • Huduma za magonjwa yasioambukiza kama Magonjwa ya moyo
 • Huduma za EMG/ICU
 • Tiba kwa mionzi pamoja na huduma za saratani

2. Kuanzisha kitengo cha utafiti na maendeleo ambacho kitakuwa kinashughulika na utafiti wa magonjwa katika mkoa na Taifa kwa ujumla, pamoja na tafiti nyingine katika sekta afya.

3. Kuanzisha chuo cha mafunzo ambacho kitasaidia kutoa wataalamu wa afya wa aina zote kwakuwa upungufu wa watumishi kwa mkoa wa kigoma ni zaidi ya asilimia 50

4. Kuongeza ukarabati wa majengo kwakuwa yaliyopo sasa mengi ni chakavu sana na hayakidhi kutoa huduma zilizo bora.

 • Jengo la wagonjwa wa nje
 • Stoo kuu ya jumla
 • Jengo la ufuaji
 • Jiko
 • Wodi namba 6 na namba 7

5.Kuongeza vyanzo mbali mbali vya mapato ikiwa ni pamoja na kuingia mkataba wa uchomaji taka na vituo vingine vya utoaji huduma, kwakuwa hospital ina High Tech Incinirator, ujenzi wa canteen ya hospital, ujenzi wa vyumba vya biashara katika eneo la hospital ambavyo vitapangishwa kwa wafanyabiashara,

6. Kufunga CCTV camera kama njia ya kuimarisha ulinzi katika hospital pamoaj na kupunguza upotevu wa mali za serikali