Historia
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma, ilianza kutoa huduma eneo hili ilipo hivi sasa mwaka 1972. Kabla ya hapo, huduma zilikuwa zinatolewa Kigoma mjini kwenye eneo ambalo hivi sasa linatumika kama kituo cha kulea watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi cha Sanganyigwa. Hospitali hii ilianzishwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wa Kigoma mjini. Hivi sasa ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambayo hupokea wagonjwa kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Kigoma pia wakimbizi na raia kutoka nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.
Hospitali ya Maweni ilipandishwa hadhi kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa tangazo lililotolewa kwenye gazeti la Serikali Na 828 la tarehe 12/11/2010. Hospitali ina uwezo wa kuchukua vitanda 300 katika wodi 11 zilizopo. Kutokana na uchakavu, wodi mbili hazitumiki, hivyo idadi ya vitanda vilivyopo wodini ni 169. Vitanda vingine 32 hutumika katika Idara nyingine kama chumba cha kujifungulia (labour room), vitanda kwa ajili ya watumishi walioko zamu za usiku na Vitanda katika vyumba vya Madaktari (examination beds).
Huduma Zinazotolewa
Huduma zifuatazo zinatolewa; wagonjwa wa nje (OPD), magonjwa mchanganyiko (internal medicine), upasuaji (surgery), magonjwa ya akinamama na uzazi (obstetric and gynaecology), magonjwa ya akili (psychiatry), magonjwa ya kinywa na meno (dental), magonjwa ya macho (opthalmology), mazoezi ya viungo (physiotherapy), dawa (pharmacy), maabara, radiolojia, Huduma za UKIMWI (CTC, PMTCT, VCT, PITC, EID, HBC) na huduma za kuhifadhi maiti.
Kwa wastani wagonjwa 150-200 hupata huduma kila siku hapa hospitalini. Kwa mujibu wa takwimu za MTUHA za mwezi Julai 2019, magonjwa kumi yanayoongoza hapa hospitalini ni;
Wagonjwa wa nje (OPD) |
B. Wagonjwa waliolazwa (IPD)
|
Upper respiratory tract infections Malaria Urinary tract infections Diabetic Mellitus Hypertension Skin infections Sexually transmitted infections Anemia. Peptic ulcer diseases Rheumatoid joint disease |
Malaria Anemia Abortion complications Hypertension Pneumonia Peptic ulcer disease Fracture Neonatal sepsis Urinary tract infection HIV infections (symptomatic) |