UGONJWA WA MARBURG NI NINI?
Posted on: August 14th, 2023Kulingana na Umoja wa Mataifa, virusi vya Marburg, ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 31 kuambukizwa, saba kati yao walikufa, mnamo 1967 huko Marburg na Frankfurt. Ujerumani na Belgrade huko Serbia.
Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kikohozi, maumivu ya viungo, kuhara na kutapika, na mara nyingi hata upungufu wa damu katika mwili.
Mlipuko huo ulitokana na tumbili wa Kiafrika walioagizwa kutoka Uganda. Lakini virusi hivyo vimehusishwa na wanyama wengine tangu wakati huo.
Na miongoni mwa wanadamu, huenezwa zaidi na watu ambao wamekaa kwa muda mrefu katika mapango na migodi iliyo na popo.
Unaanza ghafla na:
- Homa
- Kuumwa vibaya na kichwa
- Kuumwa na misuli
Hii mara nyingi siku tatu hufuatwa na:
- Kuharisha
- Kuumwa na tumbo
- Kichefuchefu
- Kutapika
Ugonjwa Wa Marburg Unaenezwa Kwa
Popo wa matunda aina ya rousette wa Misri mara nyingi huwa na virusi. Nyani wa kijani kibichi na nguruwe wanaweza pia kubeba.
Miongoni mwa wanadamu, huenea kupitia maji ya mwili na malazi yaliyochafuliwa nao.
Na hata watu wakipona, damu au shahawa zao, kwa mfano, zinaweza kuwaambukiza wengine kwa miezi mingi baadaye.
Je, Inaweza Kutibiwaje?
Hakuna chanjo maalum au matibabu ya virusi.
Vinawezaje Kudhibitiwa?
Watu barani Afrika wanapaswa kuepuka kula au kushika nyama ya porini.
Na wale wanaozika watu ambao wamekufa kutokana na virusi wanapaswa kuepuka kugusa mwili.