ZOEZI LA UPIMAJI WA SARATANI

Posted on: April 8th, 2023

Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kigoma - Maweni kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road wameendesha zoezi la upimaji wa saratani kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma, katika zoezi hilo jumla ya wananchi 405 wamechunguzwa ambao wanawake ni 339 na wanaume 66 ambao walihudhulia kwa siku 2. Pia zoezi hilo lililenga kuwajengea uwezo watoa huduma wa Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Kigoma – Maweni ili waendelea kutoa huduma za upimaji wa saratani kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma.