ZAWADI KWA WALIO FANYA VIZURI IPC MAWENI RRH ZATOLEA WAHIMIZWA MWENDELEZO
Posted on: March 27th, 2025
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma leo imetoa zawadi kwa idara zilizofanya vizuri katika masuala ya kukinga na kudhibiti maambukizi (IPC) kwa lengo la kuchochea utendaji ili kuendelea kufanya vizuri katika eneo hilo.
Maweni imekua Hospitali namba moja kitaifa kati ya Hospitali 27 za Rufaa za Mikoa mwaka 2024 hivyo katika kuhakikisha Hospitali inaendelea kufanya vizuri uongozi wa Hospitali kwa kushirikiana na kitengo cha uimarishaji ubora cha Hospitali umetoa zawadi mbalimbali kwa idara zilizo fanya vizuri na kuifanya Hospitali kushika nafasi ya kwanza kitaifa.
Mkuu wa kitengo cha uimarishaji ubora Maweni RRH Dkt. Juma Masanja, ameeleza maendeleo ambayo yamefikiwa kwa sasa, huku akisisitiza watumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi suala la huduma kwa wateja akilipa kipaumbele ambapo ameahidi kuwa kitengo cha uiamarishaji ubora itaendelea kusimamimia na kuhakikisha ubora wa huduma.
" tunatoa zawadi hizi kwasababu tumeweza kufanya kazi nzuri, na siyo idara yangu ya ubora bali ni idara mbalimbali na tumehakikisha Hospitali yetu inashika nafasi nzuri hivyo niwambie tu kwamba tunaendelea kujikita zaidi katika kutoa huduma bora lakini huduma hizo haziwezi kuwa bora bila kukinga na kudhibiti maambukizi. Amesema Dkt. Masanja.
Dr. Masanja ameyasema hayo katika utoaji wa zawadi kwa idara zilizo fanya vizuri kt eneo la IPC ambapo amesema hospitali imepiga hatua na kuwa ya kwanza kitaifa, hivyo kulingana na hilo leo zawadi zitatolewa.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt. Stanley Binagi amewataka watumishi na idara zote kuendelea kuimalisha huduma kwa ubora ili kuweza kuendelea kufanya vizuri ambapo amezitaka idara ambazo hazijafanya vizuri kuhakikisha zinafanya jitihada za makusudi ili kufanya vizuri.
“nikiuliza hapa ambaye anamjua mnyama mwenye kasi zaidi duniani wengi tunamjua lakini wa pili je? Hatujui, hivyo sisi kama Maweni tunahitaji kuwa wa kwanza na sio mbili wala tatu kwani hakuna anaye fatilia hivyo lakini kuwa namba moja inafatiliwa sana hivyo tuendelee kuboresha. Amesema Dkt. Binagi.