WATUMISHI MAWENI RRH WAPATIWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO

Posted on: March 4th, 2025

Leo tarehe 28/02/2025 watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni -Kigoma wapatiwa mafunzo ya kinga na kukabiliana na majanaga ya moto kwa lengo la kuendelea kuzuia majanga ya moto katika taasisi mbalimbali za Serikali na majumbani.

Katika mafunzo hayo yaliyo hudhuriwa na watumishi wa kada mbalimbali kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni -Kigoma ASF. Jacob S.Chacha kaimu kamanda jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Kigoma amewataka watumishi kutumia vema elimu hiyo ili kuweza kupambana na majanga ya moto katika majumba yao na wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi.

“ipo haja ya kuchukua ahatua Madhubuti kujikinga na majanga ya moto hasa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia , huku akifafanua zaidi kuhusu matumizi ya gesi ya kupikia hivyo sisi kama watumishi tanapaswa kujua jinsi gani ya kupambana na majanga ya moto tuwapo majumbani pamoja na mahala pakazi”amesema ASF.Chacha.