KAMBI YA HUDUMA ZA KIBINGWA YAZINDULIWA MAWENI RRH

Posted on: October 26th, 2024


Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya ikiwa nijitihada za Serikali  kupitia Wizara ya Afya Leo tarehe 28/10/2024 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma imeanza kutoa matibabu ya kibingwa katika kambi ya matibabu inayo wajumuisha madakitari 31 kutoka katika Hospitali mbalimbali nchini.Kambi hiyo ambayo imezinduliwa rasimi na Mkuu wa Mkoa wa kigoma Mh. Thobias Andengenye inalenga kutoa huduma kwa wananchi takribani 3500 kwa muda wa siku tano.


Aidha katika uzinduzi huo Mh. Thobias Andengenye ametoa pongezi kwa madakitari wote walioweza kufika kutoa huduma  kwa wananchi wa Kigoma pia akizishukuru taasisi mbalimbali za afya kwa kuweza kuitika wito wa kuleta wataalamu kwaajili ya kutoa huduma


“Nipende kuwashukuru sana madaktari bingwa walioweza kuungana nasi kuja kutoa huduma  na kuungana nasi katika kusherehekea miaka 50 tangu Hospitali yetu ianzishwe” Mh. Thobias Andengenye.



Pia ameendelea kusema kuwa kambi hii inaenda kuondoa adha kwa wananchi kufuata matibabu mbali na Mkoa wao, huku akiishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Mh. Rais Dkt. Samia Suruhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika Mikoa ya pembezoni na nchi nzima kwa ujumla.


“Kupitia jitihada hizi za Serikali tumepunguza mzigo wa wananchi kufuata huduma mbali, pia tunaishukuru Serikali kupitia wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha huduma za Afya katika maeneo yetu”


Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye ametoa wito kwa wananchi waKigoma kushiriki zoezi muhimu linaloendelea nchini la uchaguzi wa Serikali za mtaa ili kuweza kupata viongozi wanao weza kusimamia lasilimali zetu vizuri ili kuweza kuendelea kuboresha huduma bora kwa jamii.


“Niwaombe wananchi tujitokeze kushiriki zoezi linalo endela hivi sasa la uchaguzi wa Serikali za mitaa ili tuweze kupata viongozi wanaoweza kusimamia lasirimali zetu na simasilahi binafi” Mh. Thobias Andengenye.




Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt. Stanley Binagi  ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha Hospitali ya Mkoa Maweni – Kigoma, pia akitoa wito kwa wananchi kujiandaa na sera ya BIMA YA AFYA KWA WOTE ambapo amewataka wananchi kuhakikisha wanapata Bima hizo kwani nimuhimu sana.



“Wananchi wengi wamekua wakilalamika gharama za matibabu hivyo Hospitali imeungana na wadau mbalimbali kuweza kufanikisha hili ambapo baadhi ya wananchi wenye vigezo hupatiwa matibabu bure, pia wananchi wote wa kigoma tujiandae na Bima ya Afya kwa wote ambayo itakua garama nafuu sana na hautaona faida ya Bima ya Afya kama haujaumwa hivyo tufikilie kuwa na Bima ya Afya. Dkt. Stanley Binagi.