WANANCHI WATOA PONGEZI KWA UONGOZI MAWENI RRH KIGOMA

Posted on: August 8th, 2024

    

   Wakati ambao Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh Rais Dk.Samia Suluhu Hassani kupitia wizara ya Afya imepiga hatua katika kuboresha sekta ya afya kwa uwepo wa huduma mbalimbali na vifaa tiba wananchi mkoani Kigoma wametoa pongezi kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni -Kigoma kwa kuendelea kutoa huduma bora  huku wakibainisha kuwa kwa sasa huduma nyingi zinapatikan Hospitali ya Maweni tofauti na miaka kadhaa nyuma

     

     Getrad Stewad mkazi wa Lusesa wilayani Kasulu nimiongoni mwa waliofurshishwa na huduma katika Hospitali ya Maweni ambapo amesema kuwa kwa sasa huduma zinatolea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni zimeboreshwa sana akilinganisha na kipindi cha nyuma


‘’niseme ukweli kuwa mimi nimetokea Lusesa kuja kupata huduma nimemleta mwanangu ambaye anatatizo la mdomo wazi  sikudhani kama mwanangu angeweza kuonekana tena kama Watoto wengine kwa sababu kila niliye mshirikisha alininiambia nimipango ya Mungu , sawa nimipango ya Mungu lakini nikachukua hatua ya kumleta hapa maweni mwanangu amefanyiwa upasuaji na sasa amekua vizuri na sijalip


ia chochote’’ alisema Getrad .


     Pia ameendelea kuwaomba wazazi wenye Watoto wenye tatizo la mdomo wazi kuja Hospitali kwa sababu matibabu hayo nibure lakini hajaliacha nyuma suala la kuishukuru na kuipongeza Hospitali kwa huduma nzuri aliyopatiwa

‘’ Niwambie tu wazazi wenye Watoto ambao wanatatizo kama alilokuanalo mwanangu waje  Hospitali  ya Maweni kwa sababu huduma hii inatolewa bure kabisa lakini pia nitumie nafasi hii kutoa pongezi zangu kwa uongozi na watumishi wote wa Maweni kwa kujitoa kwa kila hali kutusaidia’’

  

  Aidha Mederina Samweli Ayubu mkazi wa ujiji  amesema amekua akipata huduma katika Hospitali ya Maweni mwaka wa kumi sasa ambapo amebainisha kuwa huduma zimekua zinaongezwa siku hadi siku  kitu ambacho kimekua chachu ya wanakigoma kuiona Hospitali hiyo kama kimbilio


‘’Kwanza tunashukuru sana tumefanikisha kupataka huduma hii nzuri kwaiyo nipende kuishukuru hospitali kwa kuendelea kutuhudumia sisi wanakigoma nimekua nikip

atiwa huduma hapa Maweni takilibani miaka kumi sasa kwakweli tupongeze viongozi wa hospitali wanafanya kazi nzuri na huduma zinakua kila kukicha ‘’amesema Mederina.


      Hata hivyo Maweni Afya Hbari ikapata wasaa wa kuzungumza na Ally Sudy Tambwe ambaye nimkazi wa Manispaa ya Kigoma ujiji ambaye ameliambia jarida la Maweni Afya Habari kuwa  anafurahishwa na jinsi huduma zinavyo tolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni na kusema  kuwa alikua anatumia dawa  za mitishamba lakini kufika kwake hospitalini hapo kumemsaidia kupata tiba sahihi na sasa anatumia dawa alizopewa Hospitali


‘’ Mimi nimekuja hapa kupima nimepima presha nimepima moyo na namshukuru Mungu presha iko vizuri  japo kunashida kidogo ya moyo ambayo tangu awali ilikua ikinisumbua na nimekua nikitumia dawa zangu za mitishamba lakini toka nimekuja Hospitali kuonana na dakitari aliniandikia dawa nimeanza kutumia zinanisaidia sana’’ amesema Tambwe .