Wananchi mkoani Kigoma watakiwa kujitokeza kupata matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya Afya ya akili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni -Kigoma
Posted on: March 4th, 2025Wananchi mkoani Kigoma watakiwa kujitokeza kupata matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya Afya ya akili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni -Kigoma wakati wa kambi ya kibingwa ya magonjwa hayo inayotalajiwa kufanyika jumatatu ya tarehe 03 /03/2025 mpaka tarehe 07/03/2025 Hospitalini hapo.
Wito huo umetolewa na Dkt. Elen E.Mbekenga, ambaye ni Daktari wa Magonjwa ya Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma kupitia kipindi cha Siku Mpya cha Main Fm akieleza kwa undani juu ya magonjwa hayo ambapo amesema wananchi wasiogope kufika Hospitalini kwani magonjwa haya yanatibika kama magonjwa mengine.
“wananchi wanatakiwa kufika hospitalini kwa lengo la kupata matibabu ya magonjwa ya Afya ya akili kwani magonjwa haya yanatibika hivyo tuondoe Imani potofu kuhusu magonjwa hayo kama ilivyo kwasasa katika jamii zetu”amesema Dkt.Elen.
Pia Dkt. Elen amebainisha tofauti ya changamoto za kawaida katika maisha na magonjwa ya Afya ya akili ambapo amesema kuwa changamoto ni hali ambayo hutokea kwa mtu na kuleta hisia Fulani, pia ameendelea kwakusema kuwa ugonjwa hutokea pale ambapo mtu hushindwa kukabiliana na hali hiyo baada ya changamoto.
“tunapaswa kutambua kuwa changamoto hutokea katika maisha ya binadamu ambapo changamoto hizo ndizo hupelekea kuwa chanzo cha ugonjwa wa Afya ya akili ambazo zinaweza kuwa kihisia,kiakili na kitabia hivyo tutambue kuwa kushindwa kukabiliana na hali inayo jitokeza baada ya changamoto ndiyo inayo weza kuitwa ugonjwa wa Afya ya akili”
Hata hivyo ametoa ushauri kwa jamii kuwa na utaratibu wa kufika Hospitalini kufanya uchunguzi wa Afya zao ikiwemo Afya ya akili,pia amewasihi kuhudhuria katika kambi ya kibingwa ya magonjwa ya Afya ya akili itakayo fanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Maweni – Kigoma