WANANCHI KIGOMA WAPATA MATIBABU YA MAGONJWA YA AKILI

Posted on: March 4th, 2025

Leo tarehe 03 Machi, 2025 wananchi wamejitokeza kufanya uchunguzi pamoja na matibabu ya magonjwa ya akili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma ikiwa ni siku ya kwanza ya kambi ya matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya Akili.

Kambi hiyo ambayo imeanza leo na kutarajiwa kumalizika tarehe 07 Machi, 2025 imekua fursa kwa wananchi kuonana na kupatiwa matibabu na Wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe.

Wananchi wote mnakaribishwa kupima ili kugundua matatizo na changamoto mbalimbali za akili.