Wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya Maweni waaswa kuboresha utoaji huduma
Posted on: February 11th, 2020Hayo yamesemwa na katibu mkuu wizara ya afya dokta Zainabu Chaula alipokutana na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa maweni mnamo siku ya tarehe 10/2/2020.
Akizungumza na wafanyakazi wote dokta Chaula amesema huduma bora ya afya itwajengea watu imani pindi wanapokuja kupata huduma hospitalini hivyo ni muhimu kwa kila mfanyakazi kufanya kazi kwa bidii. Wafanyakazi wameaswa wawe na lugha nzuri kwa wagonjwa
Pia amesisitiza kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa kuhakikisha mianya yote ya rushwa ina zuiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma zote zinazotolewa lazima zipitie kwenye mfumo wa malipo.
Dokta Chaula yupo mkoani kigoma kwa ziara ya kikazi ya usimamizi shirikishi ambayo inafanywa na wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI.