UZALISHAJI WA HEWA TIBA (OXYGEN) MAWENI RRH- KIGOMA
Posted on: August 8th, 2024Wakati ambao Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh Rais Dk.Samia Suluhu Hassani kupitia wizara ya Afya imepiga hatua katika kuboresha sekta ya afya kwa uwepo wa huduma mbalimbali na vifaa tiba sambambana na na uwepo wa kituo cha kuzalisha hewa tiba ambacho kimekua msaada mkubwa kwa wagonjwa.
Hospitali ya Rufaa Mkoa Maweni - Kigoma inazalisha hewa tiba(Oxygen) ambapo huduma za gesi zinapatikana kwa urahisi badala ya kuagiza kwenye hospitali nyingine kama ilivyokua awali, kwasasa wagonjwa wamekua wakipata tiba kwa urahisi na kuokoa Maisha ya watu kwa haraka.
Hospitali imejenga na kusimika mtambo wa kuzalisha hewa tiba ya oksijeni (oxygen plant), mradi huu umegharimu shilingi 623,369,462/= na umekamilika kwa asilimia 100 na huduma zitolewa, Mradi huu umekua msaada katika mkoa mzima na mkoa Jirani wa Katavi
Awali,hospitali ilikua inalazimika kufuata gesi ya oksijen mkoani Mwanza kilometa zaidi ya 600, uboreshaji huu mkubwa umepunguza changamoto kwa wananchi wa Kigoma ambapo awali huduma zilikua hazipatikani katika Hospitali ya Rufaa Mkoani Kigoma sasa zinapatikana kutokana na juhudi za serikali.
Mpaka sasa hospitali inauwezo wa kuzalisha mitungi 50 ya hewa tiba kwa siku huku jumla ya mitungi iliyopo ni287 kukiwa na mitungi mikubwa 350 na midogo 37 ambapo yote ni mizima na hufanya kazi kutokana na mahitaji.