Ukarabati Wa Chumba Cha X-Ray Wapamba Moto, Maweni Hospitali
Posted on: October 13th, 2019Ukarabati wa chumba cha mionzi kwa ajili ya usimikaji wa mashine mpya za Xray (Digital na dual diagnostic mashine) umeanza katika hospitali ya rufaa ya mkoa maweni. ukarabati huo unafanywa kupitia mradi wa ORIO wa awamu ya pili, ambao utachukuwa miezi mine mpaka kukamili. Wawikilishi kutoka Mradi wa ORIO na wataalumu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na watoto walifika hospitali ya Rufaa ya Mkoa, siku ya Alhamisi ya tarehe 10/10/2019, kwa ajili ya kumkabidhi mkandarasi kanzi ya ukarabati, ambapo walilisitiza kuwa mkandarasi atakiwa kiufanya kazi kwa viwango vilivyotukuka na atatakiwa kufanya kazi ndani ya muda uliopangwa.
aliongeza, kuwa hakuta kuwa na muda wa nyongeza kwa muda uliopangwa kwani kwa kipindi chote cha ukarabati, huduma zitakiuwa zimesimama, aidha mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa, alimsisitiza mkanadarasi kufanya kazi kwa weledi mkubwa akizingatia BOQ aliyokabidhiwa kwa ajili ya ukarabati huo.