UJUE UGONJWA WA MPOX NA DALILI ZAKE
Posted on: August 19th, 2024Hivi karibuni ugonjwa wa Monky Pox (MPOX) umeonekana kuwa tishio katika mataifaifa mbalimbali huku mataifa kama Burundi na Kongo yakiwa tayari yameripotiwa kuwa na ugonjwa huo.
IMPOX ni ugonjwa wa virusi unaopatikana kwa Wanyama (Nyani), kutoka na shughuli za kibinadamu ugonjwa huo umetoka kwa Wanyama na kuhamia kwa binadamu na kupelekea kuambukizana binadamu kwa binadamu .
‘’Hadi kufikia sasa nchi zenye changamoto ya ugonjwa huo ni Pamoja na Congo,Burundi,Rwanda,Kenya na Uganda kwasasa nchi ambayo imepata kifo cha mgonjwa wa M-POX ni Congo’’ amesema Dkt. Erasto.
Pia Dkt. Umoja ameeleza kuwa kunahatua kuu nne za ugonjwa huo unapokua unaanza ambapo mtu anakua amepata vimelea na kuanza kuleta dalili baadae (Incubation period) ambapo inachukua muda wa siku ishirini na moja (21) na hatua ya pili ni dalili zinazoambatana na ugonjwa na dalili hizo hazitofautiani sana na zile za malaria yani Mwili kuwa na joto kali (kuchemka) ,Mafua, Mwili kuuma au kuuma na kukereketa kwa koo pia kutokwa na Mtoki kwenye shingo au pembezoni mwa mapaja na kwenye makwapa.
‘’Dalili nyingine ni kutokwa na vipele mwili mzima ambapo dalili hio huanza siku ya nne hadi wiki mbili vipele hivyo vinaweza vikatengeneza majimaji au usaa ndani yake.Amesema Dokta’’ - Erasto Umoja
Aidha ameendelea kusema kuwa endapo ikatokea mtu asiye mgonjwa kugusana na mgonjwa wa MPOX na mwili ukiwa na michubuko itapelekea kupata ugonjwa huo, pia kua na mahusiano ya kimapenzi na mtu zaidi ya mmoja ,vilevile kwa njia ya upumuaji ukiwa umekaa na mgonjwa wa MPOX chini ya mita moja au matemate ya mgonjwa yakikurukia kwenye macho,mdomo au pua hizo ni njia zinazoweza kusafirisha ugonjwa huo na pia inashauriwa kutokula mizoga yaani nyama za Wanyama waliokufa porini mambo kama hayo husababisha ugonjwa kueneo kwa haraka sana.
Hata hivyo Dkt. Erasto ametoa angalizo kubwa kwa wakazi wa Kigoma juu ya uhatari wa ugonjwa huo na kusema kuwa hauna tiba mbadala badala yake watu wanashauriwa kujikinga ipasavyo kwa kufuata ushauri wa madaktari.