TUSAIDIENI KUPATA NYUMBA SALAMA KWA AJILI YA MANUSULA WA UKATILI WA KIJINSIA
Posted on: July 29th, 2024
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma ameiomba 0R-TAMISEMI kusaidia upatikanaji wa nyumba salama kwa ajili ya manusula wa ukatili wa kijinsia kwani imekua changamoto kubwa katika maeneo haya ambapo hali hii husababisha baadhi ya kesi kutofanikiwa kwa sababu ya baadhi ya familia kuwalazimisha Watoto au ndugu zao waliofanyiwa ukatili kubadilisha maelezo pale tu wanapo rudishwa majumbani mwao hivyo kupoteza Ushahidi.
Dkt. Binagi ameyasema hayo leo tarehe 23/07/2024 katika kikao kifupi cha majumuisho ya ziara ya naibu katibu mkuu anaeshughulikia masuala ya afya ustawi wa jamii na lishe Dkt. Charles Wilson Mahera ambaye amewakilishwa na Mkurugenzi msaidizi huduma za ustawi wa jamii Subisya Kabaje katika ziara hiyo.
‘’ Watendaji wengi wa ukatili ni watu wakaribu au ndani ya familia hivyo tunapo mtibu na kumrudisha nyumbani anarudi kwenye familia hivyo anapoenda kutoa Ushahidi Ushahidi wake unakua umesha badilika hivyo tunaiomba Serikali kuanzisha nyumba salama kwa ajili ya wahanga wa ukatili wa kijinsia kigoma’’ amesema Dkt Binagi.
Hata hivyo Dkt. Binagi ameendelea kwa kusema kuwa kama Hospitali imejipanga kuhakikisha inawasaidia wahanga waukatili wa kijinsia kwa kuwapa matibabu pia imeandaa mpango wakuwasaidia watu wasikumbane na ukatili wa kijinsia kwani itakua vizuri zaidi kuliko kusubili watu waliofanyiwa ukatili ndipo wapatiwe matibabu huenda tayari anakua ameweza kupata maradhi mbalimbali hivyo tumejipanga kufanya Kliniki tembezi na kutoa elimu juu ya jambo hilo.
‘’ sisi hapa tutachukua hatua za ziada kuhakikisha tunawasaidia wahanga ambapo tunampango wa kufanya kliniki tembezi kwa ajili ya kutoa elimu na kuzuia watu wasiathilike kwa sababu kutibu watu walioathirika na ukatili huenda tunakua tumechelewa kwani yawezekana tayari amepata maradhi tayari’’
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi huduma za ustawi wa jamii Subisya Kabaje ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma kwa kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia kupitia kituo cha msaada wa mkono kwa mkono (GBV) kilichopo hospitalini hapo huku akiwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuunga juhudi suala hilo.
‘’Muone namna gani ya kuwasaidia hawa ili waweze kuwa na bajeti ya kutoa huduma hizi hasa katika kuhakikisha tunapata nyumba salama za wahanga wa ukatili wa kijinsia kwahiyo sisi kama Serikali tumelichukua lakini wadau tusaidie kuwezesha hili’’
Pia Bi. Marium Nkumbwa Afisa ustawi wa jamii OR-TAMISEMI amesema kuwa mambo yanayo fanyika katika kituo cha mkono kwa mkono (GBV) katika hospitali ya Maweni yanafaa kuigwa na halimashauri zote kwani wanatoa huduma nzuri
‘’Suala la mwongozi linafuatwa lakini pia hata jengo lenyewe lilipo ni Dhahiri kwamba wahanga wanaweza kufika bila kuogopa na mwongozo unataka hivyo pia katika upande wa utunzaji nyaraka hasa vitabu vya manusula kwakweli vinatunzwa vizuri na Maweni inafaa kuwa mfano kwa halimashauri zote, hata kuona watumishi kama Daktari, Muuguzi na polisi wapo eneo hilo la kutolea huduma kama mwongozo unavo taka nisuala la kuwapongeza kwakweli’’
Katika kikao hicho Mganga Mfawidhi Dkt. Stanley Binagi amemaliza kwa kusema kuwa hospitali itahakikisha inaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma kwa manusula wa ukatili wa kijinsia ili kuweza kuisaidia jamii .