TUHAKIKISHE KUNA DAWATI LA HUDUMA KWA WATEJA SEHEMU ZA HUDUMA
Posted on: July 27th, 2024Mganga mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ameziagiza hospitali zote pamoja na vituo vya afya kuhakikisha kunakuwa na dawati la huduma kwa wateja pamoja na kuhakikisha miongozo ya utoaji hudma za afya ipo katika sehemu za kazi.
Hayo ameyasema leo tarehe 19 /07/2024 mkoani Kigoma katika kikao kazi cha majumuisho ya ziara aliyoifanya mkoani humo ambapo amewataka waganga wakuu wa wilaya na waganga wafawidhi kuhakikisha suala la huduma kwa wateja linazingatiwa kwa kuanzisha vituo hivyo maeneo mbalimbali sehemu za kutolea huduma.
Hata hivyo Prof. Nagu amesema kunamaendeleo makubwa yameweza kufanyika katika maeneo mbalimbali katika awamu ya sita chini ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo serikali emeboresha sana upatikanaji wa dawa na huduma za afya kwa ujumla na katika kuunga mkono juhudi za serikali kuna baadhi ya bunifu zimefanyika katika maeneo mbalimbali
‘’ Katika harimashauri ya Buhigwe nimeona jengo la mama ngojea ambalo wamejenga bila kusubili pesa kutoka Serikali kuu pia nimepita Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma wameanzisha kitengo cha utengamao pamoja na viungo bandia kwaiyo niseme kuwa hizi ndizo bunifu za kuigwa ili kuongeza mapato na tujue kua ubunifu ni nyenzo ya uongozi bora’’ amesema Prof. Nagu.
Richa ya Prof. Nagu kutoa pongezi na kuonekana kufurahishwa na mwenendo wa huduma za afya mkoani Kigoma pia amewataka wajumbe wa kikao hicho kuzingatia utoaji wa huduma bora kwani limekua likipigiwa upatu na wananchi katika maeneo mbalimbali hasa suala la huduma kwa wateja katika maeneo ya huduma
‘’Nawaomba tusimamie haya na tuwe na lugha njema na nzuri kwa wananchi na kuwapa matumaini wagonjwa hivyo nimaelekezo ya wizara kuwa kila hospitali itenge eneo la huduma kwa wateja ambapo mtu mwenye changamoto anaweza kuuliza na kupewa majibu au kuelekezwa sambamba na hilo namba za viongozi ziwekwe hadharani tuweze kufikika’’
Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan A. Rugwa-ameendelea kuwataka viongozi wa wilaya hasa waganga wakuu wa wilaya na waganga wafawidhi kuhakikisha wanasimamia watumishi wao ili kuweza kuhakikisha huduma bora kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma.