TIMU YA UTAYARI NA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO YAKAA KIKAO KUJADILI MASUALA MBALIMBALI

Posted on: July 30th, 2025

Kamati ya utayari na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma imefanya kikao kazi kujadili masuala mbalimbali.

Kamati hiyo inayoongonzwa na mwenyekiti Dkt. Boniface Kilangi imefanya kikao hicho ambacho kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katikan Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma.

Katika kikao hicho ambacho kimefanyika katika ofisi za kitengo cha ubora mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Kilangi amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuhakikisha wanatumia nafasi walizonazo kufanikisha magonjwa ya mlipuko hayana nafasi miongoni mwa wagonjwa na kila mtu ambaye anafika hospitalini kupata huduma.

"labda niseme tu kwamba sisi kama wajumbe wa kamati hii tunayo nafasi kubwa ya kuhakikisha tunapambana vikali na magonjwa ya mlipo katika hospitali yetu ili kuweza kuwalinda watu wote wanaoingia na kutoka ndani ya hospitali yetu wako salama" amesema Dkt. Kilangi mwenyekiti wa kamati.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni afisa afya mazingira wa hospitali Samweli Solomon ameseam kuwa kamati inalojukumu la kutoa elimu kwa watumishi wote pamoja ambao watawaelimisha pia watu wengine katika maeneo ya kutolea huduma jambo ambalo amesema litasaidia sana katika kukabiliana na magonjwa ya mlipo hospitalini hapo.

"Labda sasa mimi nishauri kamati nzima kwa ujumla kwamba tunalo jukumu kubwa la kuhakikisha watumishi wanapata elimu juu ya magonjwa ya mlipuko ambayo hii itaenda nkutusaidia sisi kwani watu wote katika maeneo ya kutolea huduma watafikiwa na elimu hiyo" amesema Samwel mjumbe wa kamati.
@ikulu_mawasiliano