TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TAARIFA ZINAZOSAMBAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Posted on: March 27th, 2023

Machi 27, 2023.

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma — Maweni unapenda kutoa taarifa kuhusu picha na ujumbe wa maneno unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii ukionesha picha ya mwanaume na mwanamke wakiwa katika fukwe na ujumbe wa maneno ukionesha kuwa huyo ni mtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma — Maweni

Baada ya kuona picha hiyo na ujumbe huo, Uongozi umefanya ufuatiliaji wa picha hizo na ujumbe huo, na uongozi umejiridhisha kuwa mwanaume alietajwa katika picha hiyo kwa jina la Dkt. Adolf Gwahula Sio mtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma— Maweni na hospitali haina na haijawahi kuwa mtumishi wa jina hilo.

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma - Maweni unalaani vikali kitendo hicho cha kutumia jina la Hospitali na Cheo cha Daktari Mkuu wa Hospitali kwa lengo la kumchafua kiongozi wa Hospitali na Hospitali kwa ujumla. Hivyo taarifa hiyo si ya kweli na tunaomba wananchi waipuuze, watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma- Maweni wanafanya kazi kwa weledi mkubwa na kwa kuzingatia taratibu na

Kanuni za Utumishi wa Umma.

Imetolewa na:

vvvS¯

Joseph Kafwimbi,

Afisa Mawasiliano na Uhusiano,

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma — Maweni.