NIRAHISI KUPATA VIRUSI VYA HOMA YA INI MARA KUMI YA VIRUSI VYA UKIMWI

Posted on: July 29th, 2024

Tarehe 28 julai kila mwaka dunia huadhimisha siku ya homa ya ini ambapo nchini Tanzania imefanyika jijini Dar Es Salam ikiwa nimwendelezo wa kuhakikisha ugonjwa huu hatari utapata mwarobaini hata hivyo kwa upande wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imeendelea kutoa elimu kuhusu ugonjwa huo kupitia vyombo mbalimbali vya Habari.

Mapema hii leo kupitia kipindi cha Siku mpya cha Main Fm Dkt. Onesmo Edisoni amesema kuwa Homa ya ini nimaambukizi yanayotokana na virusi vya Hepatitis A, B, C, D na E ambapo virusi vya B na C nivirusi hatari sana ambavyo vinamuweka mtu hatarini zaidi

‘’Virusi aina ya Hepatitis B na C ni hatari sana ikumbukwe kuwa ni rahisi sana kupata maambukizi ya virusi vya homa ya ini mara kumi ya virusi vya UKIMWI hivyo homa ya ini nihatari sana’’ amesema Dkt. Onesmo.

Kwa upande wake Bw. Samweli Solomoni ambaye ni Afisa afya Mazingira Hospitali ya Maweni amebainishi njia mbalimbali za maambukizi ya ugonjwa  huo akisema kuwa  homa ya ini inaweza kuambukizwa kwa kudungwa sindano iliyokwisha tumika na mtu aliye kuwa na virusi vya Hepatitis B au c, pia kwa njia ya ngono iwapo mmoja Kati Yao atakua ana virusi vya homa Ya ini, mama mjamzito Anaweza kumuambukiza mtoto tumboni au wakati anaziliwa


‘’ Njia za maambukizi ya homa ya ini zinafanana na zile za virusi vya UKIMWI ndiyo maana tunasema kuwa virusi vya homa ya ini nivyepesi kuambukizwa pia maambukizi yako juu zaidi lakini pia nihatari pia jamii inatakiwa kujua kwamba homa ya ini inaweza kuambukizwa kwa njia ya majimaji kutoka kwa mtu mmoja Kwenda kwa mtu mwingine’’.


Ikumbukwe kuwa Tanzania imeungana na Dunia nzima kuadhimisha siku ya homa ya ini duniani huku kaulimbiu ikisema ‘’Homa ya ini haisubili’’ ikiwa ni mipango ya Serikali kuhakikisha ugonjwa huu hauenei nchini ambapo kutokana na taarifa ya Shirika la Afya Dunia (WHO) limesema kuwa kila baada ya sekunde 30 mtu mmoja hupoteza Maisha kutokana na ugonjwa huo huku ikikadiliwa kuwa watu 3,500 hupoteza Maisha kwa siku moja.