MITI 200 YAPANDWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MAWENI
Posted on: February 8th, 2023Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji, Ujenzi na Mazingira na Diwani wa Kata ya Kitongoni iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Himidi Omary Himidi amepongeza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma kwa kusimamia na utunzaji wa Mazingira.
Pongezi hizò amezitoa Leo February 08, 2023 alipokuwa Mgeni rasmi akiwamwakilisha Meya wa Manispaa hiyo katika zoezi la upandaji wa Miti eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma ikiwa ni mwendelezo wa kufanya Manispaa ya Kigoma/Ujiji kuwa ya Kijani
Akihutubia wafanyakazi wa Hospitali hiyo Mgeni rasmi huyo amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji inaendelea kutekeleza Maagizo yaliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais ya Kila Halmashauri kuhakikisha inaitikia zoezi la upandaji wa Miti
Amesema kwa kipindi cha robo ya Kwanza (Julai -Septemba 2022/2023) Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kushirikiana na Wadau na Wananchi imefanikiwa kupanda miche 34, 800 ikiwa ni miti ya Kivuli na Matunda
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) Dr. Ashraf Idd Bitaliho amesema wamezindua zoezi hilo la upandaji wa miti katika eneo la Hospitali ikiwa ni kuendeleza utunzaji wa Mazingira
Kaimu Mganga mfawidhi huyo amesema katika zoezi hilo Watumishi na wafanyakazi wa Hospitali hiyo watashiriki upandaji wa miti Mia mbili (200) na inatatunzwa na Watumishi kutoka katika idara na Vitengo vya hospitali hiyo
Manispaa ya Kigoma/Ujii imekuwa ikihamasisha Wananchi katika utunzaji wa Mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji miti ambapo Manispaa hiyo imekuwa ikizalisha Miche ya Kisasa ya Michikichi na kuigawa bure kwa Wakulima na Wananchi kwa lengo la kupanda shambani, kando ya barabara na maeneo yao ya kuishi