MGANGA MFAWIDHI AISHUKURU WIZARA KWA MAFUNZO YA AFYA MAZINGIRA

Posted on: November 4th, 2024
Wizara  Afya imeendesha mafunzo kwa timu ya uendeshaji wa Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma, Mafunzo yanayolenga kujenga uwezo wa kutunza mradi wa Tanzania Martenal and Child Health project unaofadhiliwa na Banki ya Dunia kupitia Wizara ya Afya  ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Hata hivyo Mwezeshaji wa Mafunzo hayo   Bw. Adolf Kiyunge amesisitiza  kuboresha  Afya mazingira na uhusiano wa kijamii ili  kuweka mazingira rafiki na ustawi  wa  Afya ya mama na mtoto.
"Sisi kama viongozi na watumishi tunahitajika kuifundisha jamii lakini pia kuchukua hatua ili tuweza kusaidia kinamama  na watoto katika jamii zetu hivyo niwajibu wetu kulifanya hili" amesema Kiyunge.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt. Stanley Binagi ameishukuru Wizara kwa kuendelea kuleta mafunzo mbalimbali Hospitalini hapo, pia akieleza jinsi gani mafunzo hayo yatakwenda kuwa msaada kwa timu hiyo ya Hospitali katika kukabiliana na changamoto zilizokuwa zikijitokeza awali.
“Naweza nikasema nimafunzo ambayo yanaenda kuongeza ufanisi katika Hospitali yetu na kuondoa changamoto mbalimbali zilizokua zikijitokeza awali hivyo wote tuliopokea mafunzo haya basi tuyafanyie kazi ili tupige hatua mbele zaidi, amesema Dkt . Binagi.


m

+4


See insights and ads

Boost post

All reactions:Maweni Rrh