MFUMO MPYA WA eHMS SASA WAWAFIKIA WATUMISHI MWAENI RRH KIGOMA

Posted on: August 7th, 2024

Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Hoaspitali na vituo vya Afya ni jitihada za Serikali kuhakikisha mwananchi wanapata huduma bora za Afya,katika kutoa huduma bora mifumo tiba imekua nyenzo muhimu katika utoaji wa huduma hizo.

Katika kuendelea kuboresha huduma Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma wameendelea kupata mafunzo juu ya matumizi ya mfumo mpya wa eHMS ikiwa ni wiki ya pili ya mafunzo hayo .
Ambapo mfumo huo utatumika na idara mbalimbali katika Hospitali za Rufaa ili kurahisisha utendaji kazi kwa watumishi kwani mfumo tiba huo utapunguza matumizi ya karatasi.

Hata hivyo Afisa Tehama Abely Schone amesema kuwa Mfumo tiba huo utatumika kwaajili ya kutunza kumbukumbu za wagonjwa Pamoja na taarifa mbalimbali za Hospitali watumiaji wakubwa wa mfumo huo ni madaktari,wauguzi, pia ameendelea kusema Serikali inaendelea kuboresha huduma za Afya nchini kupitia teknolojia.

''Mfumo huu mpywa utasaidia katika utoaji huduma kwa ubora na kwa haraka zaidi tofauti na mfumo wa zamani wa makaratasi kwani mfumo tiba huu utamrahisishia Daktari kukusanya taarifa za mgonjwa kwa urahisi zaid''.