MAWENI RRH YAPOKEA MASHINE ZA KISASA ZA KUPIMA KIFUA KIKUU

Posted on: September 24th, 2024
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma yapokea mashine za kisasa za kupimia Kifua kikuu (TB) kutoka kwa wadau wa maendeleo Shirika la THPS.
Akipokea mashine hizo leo katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali (Maweni conference Hall) Mganga Mfawidhi Dkt. Stanley Binagi amesema kuwa mashine hizo zitasaidia kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwani zinafanya kazi kubwa kwa muda mfupi,
"mashine hizi zinaenda kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma lakini ni kwa sababu zinaweza kufanya upimaji kwa haraka, pia watanzania wanatakiwa kujua kua kipimo hiki ni bure", amesema Dkt. Binagi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Damas Kayera amesema mashine hizi zitasaidia kugundua wagonjwa wengi wapya wa kifua kikuu katika Mkoa wa Kigoma ambao watapatiwa matibabu na kupunguza maambukizi mapya katika mkoa huo.
"Tunashukuru kwa THPS kuweza kuleta mashine hizi kwani zitatusaidia kuwagundua wagonjwa wengi na kuwapatia matiba hivyo na kuhakikisha hatuna maambukizi mapya kufikia mwaka 2030.