MAWENI RRH YAENDESHA MAFUNZO ELEKEZI KWA WATUMISHI WAPYA

Posted on: August 17th, 2026

MAWENI RRH YAENDESHA MAFUNZO ELEKEZI KWA WATUMISHI WAPYA

Watumishi wapya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma, wametakiwa kupinga rushwa wakati wa utekelezaji wa majumu yao kwa wananchi.


Akizungumza wakati wa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya Katibu Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni, Bw. Odax Rukiza, ameeleza kuwa rushwa ni adui wa haki kwa kila mtu na kwamba ni uvunjifu wa maadili kwa mtumishi wa umma, kushiriki katika kutoa ama kupokea rushwa kwa wananchi ili kutoa huduma.


Ameleeza kuwa mtumishi wa umma ana wajibu wa kutekeleza wajibu wake bila upendeleo kwa mtu yeyote na bila kujali hali ya mtu isipokuwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, miiko na maadili ya utumishi wa umma.


“Hata kama utapewa zawadi na mgonjwa baada ya kumhudumia, zawadi hiyo utapaswa kuiwasilisha ofisini kabla ya kuitumia, kufanya kinyume ne hivyo wewe utahesabika ni mpokea rushwa na taratibu za kisheria zitachukuliwa juu yako na mamalaka husika” Ameeleza Odax


Mafunzo hayo yatatekelezwa kwa muda wa siku tano kuanzia leo 17 Agosti hadi 21 Agosti 2026 yakiwana lengo la kuwajenga watumishi wapya namna ya kutelekeleza majukumu yao kulingana na maadili ya utumishi wa umma ikiwa ni pamoja nakupiga vita rushwa eneo la kazi.