MAWENI RRH SIKU YA WAUGUZI DUNIANI YAADHIMISHWA KITOFAUTI

Posted on: May 14th, 2025

Ifikapo tarehe 12 Mei kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya Wauguzi ikiwa ni sherehe za kumuenzi mwasisi wa taaluma hiyo Florence Nightingale ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika mkoani Iringa na Wilani Buhigwe ngazi ya Mkoa.

Katika kuadhimisha siku hiyo wauguzi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni -Kigoma wauguzi wamejumuika Pamoja na kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa katika wodi ya wazazi Pamoja na wodi ya Watoto na kupata wasaa wakukumbushana baadhi ya mambo muhimu ya kiuguzi huku suala la majukumu ya muuguzi likizungumzwa.

“Wauguzi wezangu tupo hapa leo kuadhimisha siku ya wauguzi duniani ambao ndiyo sisi, hivyo Pamoja na kucheza kunywa na kula basi jambo la kukumbushana wajibu ni suala la msingi sana, niwaombe sasa tuendelee kutimiza wajibu wetu ili kuweza kuwahudumia wananchi kwani huu ni wito kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuimarisha afya za wananchi tunao wahudumia”amesema Joyce Kaimu Muuguzi Mfawidhi.

Pia miongoni mwa mambo ambayo yamefanyika katika maadhimisho hayo ni Pamoja na kiapo ambapo wauguzi wote wameapa kuwatumikia wananchi na kuwajibika kama wauguzi, kiapo ambacho huapa pindi wanapo hitimu masomo ya uuguzi, hata hivyo Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Dkt Ashrafu Bitaliho kaimu msimamizi wa huduma za Afya amesema ipo haja ya kada zingine kuiga kilicho fanywa na wauguzi katika siku yao.

“Leo tumeona hapa Wauguzi wamefanya jambo kubwa wametoa zawadi kwa wagonjwa lakini pia wameweza kutukutanisha hapa ili kuweza kufurahi Pamoja hivyo nitoe wito kwa kada nyingine kuiga” amesema Dkt. Bitaliho

Katika tukio hilo ambalo limeambatana na usomaji wa lisala kwa mgeni rasmi ambayo imeelza baadhi ya changamoto za wauguzi, mafanikio na mapendekezo Dkt. Ashlafu Bitaliho ameseama kuwa changamoto hizo zinaenda kutatuliwa kupitia menejiment ya Hospitali na kuwaomba wauguzi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili wakati changamoto na mapendekezo yao yakiendelea kufanyiwa kazi katika ngazi ya Hoapitali.

“Changamoto nimezisikia niahidi tu kwamba kupitia menejiment ya Hospitali zitafanyiwa kazi hivyo tuendelee kufanya kazi kwa kujitoa na kuzingatia maadili kama ambavyo tumekula kiapo” amesema Dkt. Bitaliho.