MAFUNZO YA UONGOZI KWA WAKUU WA IDARA 2023
Posted on: February 24th, 2023Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni yatoa mafunzo ya Uongozi kwa wakuu wa idara na vitengo 50, mafunzo hayo yameandaliwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni na yanafundishwa na wawezeshaji kutoka Wizara ya Afya na chuo cha mafunzo CEDHA (Center for Educational Development in Health/Arusha. Mafunzo hayo yameanza kutolewa tarehe 20/02/2023 na yanatarajiwa kukamilika tarehe 03/03/2023.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma – Maweni Dkt. Lameck Mdengo alieleza mafunzo hayo yataisaidia Timu ya Usimamizi na Uendeshaji wa huduma za afya ya Hospitali katika kupanga na kusimamia shudhuli mbalimbali za hospitali Ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi ambayo inakwenda sambamba na kusimamia vifaa tiba, dawa, watumishi na miundombinu ya Hospitali kwa ujumla.