MAFUNZO YA UANDAAJI WA BAJETI YAFIKIA SIKU YA PILI

Posted on: January 16th, 2026

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imeanza maandalizi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu wa kuandaa bajeti kuanzia ngazi ya vitengo na idara, ambapo awali mafunzo ya uandaaji yametolewa kwa wakuu wa idara na vitengo tarehe 13 mwezi Januari, 2026.

Katika kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa kuzifikia idara na vitengo mbalimbali tayari kamati ya mipango ya Hospitali imeanza kufanya mafunzo kwa idara mbalimbali zikiwemo, Utawala,Upasuaji,Maabara,Radiolojia pamoja na idara ya Magonjwa ya Dharura na Wagonjwa wa Nje zikiwa katika kundi la kwanza ambalo idara hizo zimepata mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 14 hadi 15 Januari, 2026.

Hata hivyo idara nyingine zitaendelea kupatiwa mafunzo hayo tarehe 16 hadi tarehe 17 Januari,2026 zikiwa kwenye kundi la pili la mafunzo, hata hivyo kamati ya mipango kupitia Kaimu mwenyekiti wake Bw. Joseph Kafwimbi amewataka washiriki wote kutilia maanani mafunzo hayo huku akieleza kuwa ushiriki kikamilifu utaleta tija kwa taasisi na kufikia lengo.

“ Nipende kusema kwamba inatupasa watu wote ambao tumepangwa kushiriki mafunzo haya tushiriki lakini pia siyo kushiriki tu bali ni kushiriki kikamilifu, wasiwepo washiriki ambao wanafikili jambo hili siyo muhimu na kuondoka kabla ya kumaliza kwa zoezi zima, wote tushiriki ili tuweze kufanya jambo kwa ubora ili kuweza kuleta tija kwa taasisi” amesema Kafwimbi Kaimu Mwenyekiti.