MAFUNZO UANDAAJI WA BAJETI MAWENI RRH YAFIKIA TAMATI

Posted on: January 17th, 2026

Leo tarehe 17 Januari,2025 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imetamatisha mafunzo ya maandalizi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa idara zote Hospitalini hapo lengo likiwa ni kuhakikisha kila idara inawezakuandaa bajeti yake katika mwaka wa fedha 2026/2027 ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu wa kuandaa bajeti kuanzia ngazi ya vitengo na idara.

Hapo jana tarehe 16 Januari,2026 mafunzo yametolewa kwa idara ya Magonjwa ya wanawake na uzazi, Idara ya Watoto, idara ya Famasi, pamoja na idara ya Physiotherapia,na kuendelea hii leo ambapo zimekua idara za mwisho kupatiwa mafunzo Hata hivyo idara hizo ndizo zinakamilisha utaratibu wa mafunzo yaliyopangwa kutolewa kwa siku nne kwa idara zote.

Hata hivyo baada ya mafunzo hayo kila idara itaweza kuandaa bajeti yake ambayo itawasilishwa katika kamati ya Mipango ya Hospitali ili kuweza kuandaa bajeti ya Hospitali kwa ujumla.