MAADHIMISHO YA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MAWENI
Posted on: October 18th, 2022Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma - Maweni inawatangazia wananchi kuwa inategemea kuadhimisha kilele cha kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake na kutoa huduma za Afya, katika kuadhimisha kilele cha kutimiza miaka 50, Hospitali imepanga tarehe 20 na 21/10/2022 itatoa huduma za uchunguzi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kutoa elimu ya afya kwa wananchi, gharama za kuwaona madaktari hazitakuwepo. Hivyo mwananchi atagharamia vipomo na Dawa tu kama itaonekana kuna umuhimu wa huduma hizo, Hospitali imepanga kutumia madaktari bingwa waliopo Maweni Hospitali katika kutoa huduma hizo ambao ni kama ifuatavyo;
Daktari Bingwa wa Huduma za kina mama na uzazi,
Daktari Bingwa wa Upasuaji,
Daktari Bingwa wa Mifupa,
Daktari Bingwa wa Watoto,
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani (Presha, Kisukari na Mengineyo),
Daktari Bingwa wa Huduma za dharura,
Wataalamu bobezi wa Viungo Bandia na Mazoezi Tiba (physiotherapy),
Madaktari wa Huduma za Kinywa na Meno,
Huduma zingine ni Upimaji wa saratani ya Mlango wa Kizazi na Upimaji.
Pia katika kilele hicho cha kutimiza miaka 50 Hospitali itaadhimisha siku ya afya ya macho Duniani kwa mwaka 2022, ambapo huduma mbalimbali za macho zitatolewa. Wananchi wote mnakaribishwa Maweni Hospitali ili mpate huduma mbalimbali za afya na tuadhimishe kilele cha kutimiza miaka 50 ya Hospitali yetu kwa pamoja.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo:-
Mratibu wa Huduma za matibabu - 0658777415
Afisa Uhusiano wa Hospitali – 0753528030