MAABARA YETU
Posted on: September 22nd, 2024
Maabara ni mahali ambapo kuna vifaa na zana za kufanyia majaribio na uchinguzi wa kisayansi. Kwa kawaida, ni sehemu ambapo watafiti na wanafunzi hufanya kazi. Maabara zinaweza kuwa sehemu muhimu sana katika kufanya utafiti na kuelewa mambo mbalimbali. Maabara za Hospitali ni sehemu muhimu sana katika huduma za Afya. Historia yake inaonosha kuwa maabara za Hospitali zilianza kuwa muhimu zaidi karne ya 19 wakati wa maendeleo ya tiba ya kisasa.
Maabara hizi hutoa huduma za uchunguzi wa maabara kama vile vipimo vya damu, mkojo, na vipimo vingine vya kisayansi vinavyosaidia madaktari kutambua magonjwa na kutoa matibabu sahihi kwa wagonjwa. Maabara za Hospitali zina vifaa vya hali ya juu vinavyowezesha uchambuzi wa haraka na sahihi wa sampuli za wagonjwa.
Kutokana na maendeleo ya Sayansi na teknolojia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni-Kigoma ni miongoni mwa Hospitali zenye maabara za kisasa zinazotoa huduma bora kwa watanzania hususani kwa mkoa wa Kigoma ambapo wananchi kutoka sehemu mbalimbali wamekua wakipata huduma ya vipimo katika maabara hio.
Ikumbukwe kuwa awali Hospitali ilitoa huduma ya vipimo vidogo na hapa nazungumzia miaka ya 1972 hadi kufikia miaka ya 2000 kabla ya hospitali hiyo kupandishwa hadhi kua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma mwaka 2010 katika tangazo lililochapishwa kwenye gazeti la Serikali.
Maabara hiyo imekua msaada mkubwa sana kwa wakazi wa Kigoma na nchi za Jirani mfano Burundi Pamoja na Congo kwa kutoa huduma bora zenye hadhi ya Mkoa, baadhi ya vipimo ambavyo hufanyika ni kama vile Hormon Profile, RBG, Urea nitrogren, ALP, dDimer.