MAABARA MAWENI RRH YAENDELEA KUSIMIKA MIZIZI YA UBORA
Posted on: February 3rd, 2026Idara ya Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imeendelea kuboresha huduma zake kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma huku vipimo na huduma mpya mbalimbali zikianza kutolewa tofauti na ilivyokua hapo awali na kutunukiwa cheti cha ubora na Southen African Development Communityn (SADICAS)
Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha mwaka cha idara hiyo ambacho kimelenga kujadili mafanikio, changamoto na mwenendo wa utoaji wa huduma katika idara hiyo, kikao ambacho kimehudhuliwa na wajumbe kutoka kitengo cha Ubora wa huduma Hospitalini, idra ya Utawala Wakuu wa idara mbalimbali pamoja na wauguzi viongozi.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mwenyekiti Bw. Siraji Shumbusho amesema idara ya maabara imekuwa miongoni mwa idara ambazo zinafanya vizuri ngazi ya taifa katika ubora wa huduma ambapo amesema kuwa mwaka 2025 maabara hiyo imetunukiwa cheti cha ubora kutoka (SADICAS) huku akibainisha kuwa katika maabara hiyo kitengo cha Damu salama kimekuwa cha Kwanza Kitaifa katika ukusanyaji wa damu za Kuongezea watu wenye upungufu wa damu.
“Tunaendelea kufanya vizuri na kuweka nguvu, matunda kama haya Damu salama kuwa ya kwanza katika ukusanyaji wa damu za kuongezea watu wenye kuhitaji ni jambo ambalo linapendeza hivyo tunajadili hapa ili tuendelee kuwa bora Zaidi”amesema Shumbusho.
Hata hivyo Bw. Shumbusho amewaomba watumishi wa idara hiyo kupitia kikao hicho kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Kigoma.



