KWA MARA YA KWANZA MAWENI RRH YAFANYA UPASUAJI KUBADILISHA NYONGA
Posted on: May 30th, 2025
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma yatoa huduma ya upasuaji kwa mgonjwa mwenye tatizo la nyonga kwa mara ya kwanza ikiwa ni siku ya tano ya kambi ya matibabu ya kibingwa na Ubingwa Bobezi katika hospitali hiyo.
Akizungumza na vyombo vya Habari Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dk. Joseph Nangawe amesema wananchi hawanabudi kufika kupata huduma hiyo kwasababu wataalamu wako makini, pia mgonjwa huandalia kwa umakini kuhakikisha anapata huduma bora.
“Hospitali na timu nzima ya upasuaji imefanya mandalizi ya kutosha kwanzia kuingia hospitali, hivyo niwahakikishie wananchi kuwa huduma hii ni salama lakini pia niendelevu na leo niupasuaji wa kwanza katika hospitali yetu” amesema Dk. Nangawe, Kaimu Mganga Mfawidhi.
Pia Dk. Nangawe amesema kuwa jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Dk. Samia Suluhu Hassan zimeendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa kuwapeleka madaktri Bingwa na Bobezi katika hospitali za kanda Pamoja na hospitali za rufaa ambao wanasaidia sana kutoa huduma kwa wananchi.
“Hizi ni jitihada za Serikali yetu ya awamu ya sita ambayo imekuwa ikileta madakitari Bingwa na Bobezi katika hospitali zetu za rufaa hii ndiyo sababu ya hiki kinacho fanyika hapa leo” amesema Dk. Nangawe.
Hata hivyo Dk. Wilson Masanja ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya mifupa kutoka Hospitali ya Kanda Bugando Mwanza amesema, katika kambi hii ya siku tano huduma ya kumbadilishia nyonga kwa mgonjwa ambaye amesumbuliwa na tatizo la nyonga kwa muda mrefu imefanyika huku akitoa wito kwa wananchi kutumia Hospitali ya Maweni kupata huduma hizo kwani kuzifata mbali nigharama kubwa.
“Mala nyingi huduma hizi ninapatikana katika hospitali kubwa za kanda lakini leo tumefanikiwa kufanya upasuaji huu mkubwa hapa, niupasuaji wa kwanza hapa Maweni hivyo wananchi wafike kupata huduma ” amesema Dk. Masanja.
Dk. Masanja ameendelea kusema kuwa upasuaji ambao umefanyika leo umefanyika kwa asilimia 100 ambapo matibabu hayo yamefanyika ili kumtoa mgonjwa kitandani hivyo atarudi katika haliyake ya kawaida na kutatembea.
@wizara_afyatz
@ikulu_mawasiliano
@kigomars
@kigomaujijimc