KITENGO HUDUMA KWA WATEJA CHABORESHWA ZAIDI
Posted on: September 23rd, 2024
Katika ziara ya Mganga Mkuu wa serikali Mkoani Kigoma Juni 2024 alizitaka Hospitali zote na vituo vya Afya nchini kuhakikisha kua dawati la huduma kwa wateja linakuwepo katika sehemu za kutolea huduma lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi kupata maelekezo na usaidizi wafikapo katika vituo hivyo.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imeendelea kuboresha dawati la huduma kwa wateja kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa Kigoma na maeneo Jirani wanapata huduma bora wafikapo Hospitalini hapo.
Nae Mtoa huduma kwa wateja Ezekieli Thogomba “amesema kuwa mgonjwa afikapo Hospitalini hapo atapokelewa na dawati la huduma kwa wateja na kupelekwa Mapokezi kwa ajili ya kujisajili kwenye mfumo na kwenda kuonana na Daktari kwa ajili ya kuendelea kupata huduma”.
Pia bwana Thogomba ameeleza kuwa “kwa wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya huduma zinazotolewa jengo la OPD vilevile kwa wagonjwa wa dharura wafikapo Hospitalini hapo watapokelewa na kupatiwa huduma kwanza na taratibu nyingine zitafuata”.