KATIBU TAWALA MKOA WA KIGOMA AZUNGUMZA NA WATUMISHI MAWENI RRH

Posted on: October 4th, 2024

Leo tarehe 3 /10/3024 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mh. Hassan A. Rugwa ameitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni -Kigoma na kupata wasaa wa kuzungumza na watumishi hospitalini hapo.

Mh. Hassan A. Rugwa amefanya kikao kazi na watumishi hao lengo likiwa ni kusikiliza maoni, mapendekezo ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma hata hivyo ameahidi kuyafanyia kazi maoni ya watumishi ili kuwajengea mazingira Rafiki ya kufanya kazi na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma.

Pia Mh. Rugwa amesema miongoni mwa maoni na maombi ya watumishi nikuimalishwa kwa barabara ndani ya Hospitali ili kuimalisha huduma.

"Nikweli nimeyachukua yote ambayo mmeyaomba hivyo kwa upande wamiundombinu ya barabara ntawaleta wataalamu kuja kuangalia na kufanya tathimini ya awali". Amesema Hassan Rugwa.

Ameongeza kusema kuwa suala la kuwapa kipaumbele cha ajira wale wanaofanya kazi kwa mikataba linaangaliwa kwa ukaribu hivyo linafanyiwa kazi.

Pamoja na hayo jengo la huduma ya mama na mtoto nimiongoni mwa mambo ambayo yametajwa kuwa changamoto ambapo amesema pia litafanyiwa utekelezaji .

Hata hivyo amehitimisha kwa kutoa pongezi kwa watumishi na uongozi mzima wa Hospitali kwa kuendelea kufanya kazi nzuri na kuwaomba waendelee kufanya kazi kwani watanzania wanahitaji huduma .

" naomba nitumie kikao hiki kwa niaba ya serikali kuwapongeza kwa kazi nzuri hivyo tuendelee kufanya kazi kwa kujitoa ili tuwahudumie watanzania " amesema Rugwa.