KAMBI MAALUM YA MATIBABU MKOMBOZI KWA WAKAZI WA KIGOMA

Posted on: May 8th, 2024

Madaktari Bingwa 60 wameanza kutoa huduma za afya za kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni ikiwa ni siku ya kwanza ya Kambi maalum ya matibabu na Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh.Salum Kali amewataka madaktari hao kutoa huduma na kuainishi magonjwa yanayowasumbua wananchi ili kujua jinsi ya kuongeza huduma kulingana na uhitaji.

Katika kambi hiyo wananchi  wanatarajia kupata matibabu  ya magonjwa mambalimbali ya Moyo, upasuaji,mifupa, kinamama na uzazi na mengine mengi hivyo wametakiwa kutumia fursa hiyo.

Naye daktari bingwa Kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Serafini Patrice amesema kuwa hapo awali walikuwa wanafanya kambi mojamoja kwa kila hospitali katika kanda ya Magharibi lakini kwa sasa wanafanya kwa kushirikiana kama timu katika hospitali za kanda ya magharibi.