JAMII YATAKIWA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UGONJWA WA INI
Posted on: August 4th, 2025
Daktari wa magonjwa ya ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa maweni - Kigoma Dkt. Sylivia Urio ametoa elimu kuhusiana na ugonjwa wa homa ya Ini, na kueleza kuwa Ini lina umuhimu mkubwa kwenye maisha ya binadamu huku akibainisha kazi za Ini kwenye mwili wa binadamu.
Urio ameeleza hayo kupitia kipindi cha Good Morning cha Joy FM na kuendelea kusema, homa ya ini huambikizwa na virusi ambavyo vipo kwenye makundi matano A, B, C, D, na E ambapo virusi aina ya B, C na D huambikizwa kwa njia sawa na magonjwa ya ngono kama VVU, kuchangia sindano, kujamiana na mtu mwenye maambukizi ya virus vya homa Ini na majimaji kama jasho kumpata mtu mwingine mwenye kidonda au mchubuko sehemu ya mwili.
“Ini ina kazi nyingi zaidi ya 500 moja yake ikiwa ni kuchuja nakuondoa sumu za mwili, na dalili za Homa ya Ini ni kula chakula chenye uchafu ,kujamiana na mtu ambae ana maambukizi ugonjwa huo, kutumia damu yenye virusi vya Homa ya Ini , pia mama anaweza kumuambukiza mtoto pindi anapojifunguaa.
Aidha ameleza dalili za ugonjwa wa homa ya ini ambazo ni homa na kupoteza hamu ya kula., kichechefu na kutapika , mwili kuuma, mkojo kuwa na rangi ya njano pamoja na kupata manjano kwenye macho ,viganja vya mikono ,kucha au mwili mzima ambapo ameendelea kueleza kuwa ugojwa huo unachanjo kwa watu wazima na watoto.
“kuna chanjo tatu ambazo unatakiwa kuchanjwa kabla ya kuumwa ili kuwa na kinga mwili kuepusha ugonjwa wa Homa ya Ini, chanjo hizi hutolewa baada ya kupima lakini ndiyo maana tupo hapa leo ili kuweza kuwaelimisha wananchi kuhusiana na homa ya Ini, jinsi ya kujikinga na namna ya matibabu”amesema Urio Dkt. Magonjwa ya ndani.
Vilevile daktari Sylvia urio ametoa wito Kwa jamii kujitokeza kupima afya mala kwa mala na kupata chanjo kuhakikisha ugonjwa wa homa ya ini unatokomea kama ulivyo mpango wa Serikali kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha ugojwa huo unakwisha ifikapo 2030 huku akiitaka jamii kuachana na tabia za unyanyapaa kwa wagonjwa wa Homa ya Ini.
“Niwaombe wananchi kutowanyanyapaa wagonjwa wa Homa ya Ini bali familia ionapo mgonjwa wa aina hiyo basi afikishwe hospitali, pia jamii iendelee kuchukua hatua kupima afya ili kuepukana na ugojwa huu hatali” Amesema Urio.