HUDUMA YA KUSAFISHA DAMU (HAEMODIALYSIS) YAANZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MAWENI

Posted on: May 11th, 2021

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni anapenda kuwatangazia kwamba huduma ya kusafisha damu (HAEMODIALYSIS) inafanyika hospitalini hapa kwa sasa. huduma hii ni kwa wale wagonjwa wenye matatizo ya figo ambao wanahitaji kusafishwa. 

Huduma hii itasaidia  kupunguza usumbufu kwa wagonjwa waliokuwa wakisafiri kwenda mikoa mingine kwa ajili ya huduma hii. Hii itapunguza pia gharama za usafiri na usumbufu wa hapa na pale.