DAWA MAWENI RRH SIYO TATIZO

Posted on: September 22nd, 2024

Dawa ni huduma inayolenga kutoa msaada wa kimatibabu kwa jamii, hii inajumuisha ushauri wa dawa, huduma za Afya ya jamii, na elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa, ni sehemu muhimu ya kusaidia jamii kuhusu masuala ya Afya, hudumaa hii inasaidia jamii  kwa kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi sahihi ya dawa, kuelimisha jamii kuhusu magonjwa na jinsi ya kuzuia.

Maneja wa dukaDuka la dawa (Community pharmacy) Mwita Wambura ameliambia Jarida la Maweni Afya Habari kuwa duka la dawa la jamii linasaidia kuhudumia wagonjwa kwa makundi tofautitofauti na limekua msaada mkubwa kwa wananchi.

‘’Duka letu linahudumia watu wa makundi tofauti kwa wale ambao wanakosa dawa wanaotokea nje ya kituo wanapata huduma za dawa na vifaa tiba kwa kununua, lakini pia kwa wale ambao wamepata maelekezo kutoka kwa daktari anapaswa kufuata utaratibu kwa kununua dawa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa- Maweni, emesema Wambura.

Pia ameendela kusema kuwa kwa kutekeleza hilo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni-Kigoma mwaka 2021 ilianzisha duka la dawa Hospitalini hapo hivyo ilisaidia katika utoaji wa huduma bora kwa wateja, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Hospitali hiyo imejiandaa kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana kama mwendelezo wa utoaji huduma bora kwa wananchi. 

“Malengo ya kuanzisha duka ni kusaidia kutoa huduma bora za Afya kwa kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za Afya kwa wananchi ndani na nje ya kituo pia lengo la pili ni kusaidia na kupunguza gharama za upatikanaji wa huduma mgonjwa anapokosa dawa ndani ya kituo” Amesema Meneja wa duka la dawa Hospitali ya Rufaa Mkoa Maweni-Kigoma Mwita Wambura.

Vilevile amelieleza jarida kuwa wakati mwingine mteja anapatiwa muda anapopata changamoto yoyote na kupiga simu kupata maelezo zaidi yanayohusiana na duka ambapo akipiga muda wowote masaa 24 anaweza akapewa msaada wa haraka kwa namba zetu.

 ‘’Katika hili tunazo namba za simu   ambazo ni 0733001615 namba hii ukipiga muda wowote unaweza ukasaidiwa hata kama uko mbali na umekosa dawa katika kituo chochote mkoani hapa, tunahudumia pia wagonjwa au vituo vingine na kwa mwaka huu tumehudumia baadhi ya wagonjwa wanaotoka katika vituo vingine Ujiji Health Center na wagonjwa ambao wamehudumiwa katika kituo cha Kabanga wakakosa dawa hivyo wanalazimika kuwasiliana na sisi ambapo sisi tunawatumia dawa hizo,, Amesema Wambura.