CHF Iliyoboreshwa ni suluhisho la Misamaha ya Matibabu Hospitalini

Posted on: October 12th, 2019

BIMA ya Afya Ya jamii maarufu kama CHF yaja kama mkombozi mahospitalini, hayo yamezungumzwa siku ya Ijumaa ya tarehe 11/09/2019 na Afisa Usatawi wa jamii wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni wakati alipokuwa anatoa elimu ya CHF iliyoboreshwa kwa watumishi wa hospitali hiyo. Aidha Afisa huyo amewataka watumishi kuwashawishi wateja waweze kujiunga na Bima ya afya hiyo ili waweze kupata matibabu kwa urahisi.

CHF iliyoboreshwa itatumika mpaka ngazi ya Hospitali ya mkoa, hivyo itakuwa suluhu kwa Mismaha inayotolewa kwa wagonjwa kwa sasa na itapunguza mzigo kwa hospitali. "Ni jukumu letu sisi watumishi kuhakikisha tunatumia nafasi tulizonazo kuwashawishi wateja na wananchi kwa ujumla waweze kujiunga na BIMA hii, kwakuwa wananchi wengi wana imani kubwa sana na watoa huduma za afya" hayo yalisemwa na Afisa huyo katika ya kipindi katika ukumbi wa macho hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni.

Mafunzo hayo yalifungwa mnamo mifda ya saa 2:30 asubuhi na kuwaambia watumishi kuwa zoezi la usajili likikamilika, basi hatua inayofuata ni kuwaelekeza watoa huduma moja kwa moja, hivyo mjiandae kuwahudumia wananchi kwa kuwa sasa watakuja kwa wingi sana