BODI YA USHAURI YA HOSPITALI MAWENI RRH YAJADILI UTEKELEZAJI MIRADI MBALIMBALI
Posted on: July 22nd, 2025
Bodi ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imekaa kikao kujadili mwenendo wa utoaji huduma pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika hospitali hiyo.
Kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mokutano wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma kimelenga kujadili utekelezaji wa bajeti na maendeleo ya miradi mbalimbali katika katika robo ya mwaka 2024/2025.
Hata hivyo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kaimu katibu wa kamati ya mipango ya hospitali ameeleza kuwa 2024/2025 hospitali imetekeleza shughuli 75 kati ya 110 zilizo kuwa zimepangwa kutekelezwa ambayo ni sawa na 68% huku akibainisha changamoto mbalimbali zilizo pelekea shughuli mbalimbali kutotekelezwa huku swala la upungufu wa fedha likiwa sababu kubwa.
“mwenyekiti katika shughuli hizo idara ya utawala imeweza kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwa ni idara iliyotekeleza mipango mingi kuliko idara nyingine zote mipango hiyo nipamoja na kulipa mishahara ya watumishi na kuwasomesha watumishi” amesema kaimu katibu Boniphace.
Katika kikao hicho miongon mwa yalio zungumzwa ni upatikanaji wa wadau wa maendeleo ilikuweza kusaidia hospitali katika utekelezaji wa maendeleo ambapo wajumbe mbalimbali wametoa ushauri kwa uongozi wa hospitali kuwashirikisha wadau katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
“nashauli sasa bodi hii ya hospitali tunao uwezo kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali tutoke ili kuweza kuwatembelea wadau ili tuweze kufanya maendeleo katika hospitali yetu” amesema muhandishi Choma.
katika mjadala huo mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa katika kikao hicho Estomih Nathanael ameeleza kuwa ofisi yake inawapokea wadau wengi katika mkoa hivyo jaombo kumbwa nikuhakikisha tunatafuta njia ya kuweza kuongea nao ili kuweza kupata ushirikiano.
“Basi nimepokea hili, kama ofisi na tutaweza kulifanyia kazi kwani nijambo muhimu lamaendeleo katika hospitali yetu hii mala kadha uongozi wa hospitali umekua ukitushirikisha mambo mabilimbali hivyo tutaendelea kushirikiana ili kuweza kuhakikisha yale tuliyoyakusudia kama Mkoa na hospitali yanafanikiwa, amesema Nathanael.
Hata ivyo katibu wa afya wa hospitali ndugu ayubu charlse amesema hospitali imekuwa ikiwahusisha wadau katika shuguli mbalimbali za hospitali hivyo hili jambo likipata nguvu kubwa kutoka katika bodi hii basi tutapiga hatua za maendeleo.
“mimi niunge mkono jambo hili kwani hata kakatika shuguli mbalimbali tumekuwatukiwahusisha wadau na wame kuwa wakitusaidia hivyo tukiweka nguvu katika hili basi tutaweza kufanya vizu vizuri katika miradi mbalimbali tunayo itarajia kuitekeleza amesema Ayubu Charlese.
Pia suala la utekelezaji wa mipango ya hospitali limekuwa miongoni mwa mambo yaliojadiliwa katika kikao hicho ukiwasilisha taarifa hiyo kaimu katibu wa kamati ya mipango ya hospitali ndugu boniphace ameeleza jinsi gani hospitali imeweza kutekeleza shughuli mbalimbali za hospitali.
“katika mwaka watumishiricha richa ya changamoto za fedha huku vifaa tiba na dawa linapewa kipaumbele sambamba na mifumo yote yautoaji wa huduma”amesema boniphace.